Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 23, 2024 Local time: 18:46

Russia yasema uhusiano wake na Uingereza unaweza kuzorota chini ya uongozi wa waziri mkuu mpya


Waziri mkuu mpya wa Uingereza Liz Truss
Waziri mkuu mpya wa Uingereza Liz Truss

Russia Jumatatu imesema haifuti uwezekano kuwa uhusiano wake na Uingereza usio mzuri utakuwa mbaya zaidi chini ya uongozi wa waziri mkuu mpya.

Waziri wa mambo ya nje Liz Truss ambaye kwa miezi kadhaa amekuwa akibezwa na Moscow, amemshinda mpinzani wake Rishi Sunak, katika kuwania wadhifa wa waziri mkuu nchini Uingereza, kumrithi Boris Johnson.“

Ninaweza kusema kwamba mambo yanaweza kubadilika na kuwa mabaya zaidi, kwa sababu ni vigumu kufikiria jambo lolote baya, msemaji wa Kremlin Dmitry Peskov amesema alipoulizwa ikiwa Moscow inatarajia mabadiliko yoyote katika uhusiano na Uingereza.

Waziri mkuu anayeondoka madarakani Boris Johnson amekiomba chama cha Conservative kumuunga mkono asilimia kwa 100 mrithi wake Liz Truss, wakati akimpongeza katika ujumbe kwenye Twitter.

Johnson atawasilisha rasmi barua yake ya kujiuzulu kesho Jumanne kwa Malkia Elisabeth wa pili.

XS
SM
MD
LG