Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Mei 29, 2024 Local time: 10:39

Russia yasema sio mzaha kutaka kutumia silaha za nuclear


Jengo lililoharibiwa kutokana na mashambulizi ya Russia nchini Ukraine. April 24 2022. PICHA: AP
Jengo lililoharibiwa kutokana na mashambulizi ya Russia nchini Ukraine. April 24 2022. PICHA: AP

Waziri wa mambo ya nje wa Russia Sergei Lavrov ameyaonya mataifa ya magharibi kwamba yasichukulie kwa mzaha hatari kubwa iliyopo ya nchi hiyo kutumia silaha za nuclear dhidi ya Ukraine.

lavrov ameongezea kwamba anaona kama muungano wa NATO unajihusisha katika vita dhidi ya Russia kwa kuipatia Ukraine silaha

Lavrov alisema hayo katika mahojiano na televisheni ya serikali ya Russia.

Amesema kwamba msingi wa makubaliano yoyote kwa ajili ya kumaliza vita nchini Ukraine utazingatia na hali ya kijeshi itakavyokuwa nchini Ukraine.

Waziri huyo wa mambo ya nje wa Russia amesema kwamba Russia inajaribu kwa kila njia kuhakikisha kwamba silaha za nuclear hazitumiki kabisa katika vita hivyo.

Uvamizi wa Russia dhidi ya Ukraine ndio mkubwa zaidi kuwahi kutoka Ulaya tangu mwaka 1945, ambapo maelfu ya watu waliuawa, kujeruhiwa, miji kuharibiwa vibaya na zaidi ya watu milioni 5 kuhamia nchi zingine.

Moscow imesema kwamba hatua yake ni oparesheni maalum yenye lengo la kuipokonya Ukraine silaha na kuilinda. Ukriane na mataifa ya magharibi yametaja uvamizi huo kuwa uchokozi dhidi ya nchi huru.

XS
SM
MD
LG