Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Juni 13, 2025 Local time: 12:29

Russia yaitaka Ukraine kukubali masharti yake kabla ya kusitisha vita


Kutoka kushoto, Rais wa Russia Vladimir Putin na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy. (Picha na AP)
Kutoka kushoto, Rais wa Russia Vladimir Putin na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy. (Picha na AP)

Russia inaitaka Ukraine iache hatua za kijeshi, ibadilishe katiba yake isiegemee upande wowote, ikiri kuwa Crimea ni eneo la Russia na kutambua Jamhuri za wanaotaka kujitenga za Donetsk na Lugansk kama maeneo huru, amesema hayo msemaji wa Kremlin Dmitry Peskov.

Peskov ameliambia shirika la habari la ROITA kwamba Russia imeiambia Ukraine kuwa iko tayari kuachana na hatua zake za kijeshi kwa muda kama Kyiv itakubali madai yake.

Ilikuwa ni taarifa ya wazi zaidi ya Russia hadi sasa ya masharti ambayo inataka kuilazimisha Ukraine kusitisha kile ilichokiita operesheni yake maalum ya kijeshi nchini Ukraine ambayo sasa imeingia siku ya 12.

Peskov amesema Ukraine ina taarifa kuhusu masharti hayo. Na waliambiwa kwamba hili linaweza kusitishwa kwa muda. Kuhusu suala la kutopendelea upande wowote alisema,

“wanapaswa kufanya marekebisho ya katiba kulingana na mambo ambayo Ukraine inakataa malengo yoyote ya kuingia katika taasisi yoyote.

Hili linawezekana tu kwa kufanya mabadiliko ya katiba.” Msemaji wa Kremlim alisisitiza kuwa Russia haitaki kutoa madai yoyote zaidi juu ya Ukraine.

XS
SM
MD
LG