Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Oktoba 11, 2024 Local time: 02:26

Russia yaishtumu Marekani kuwanyima visa waandishi wake wa habari, Moscow yaahidi kulipiza kisasi.


Waziri wa mambo ya nje wa Russia Sergey Lavrov akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari mjini Havana, Cuba, Aprili 20, 2023.
Waziri wa mambo ya nje wa Russia Sergey Lavrov akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari mjini Havana, Cuba, Aprili 20, 2023.

Russia Jumapili ilisema kwamba Marekani imewanyima visa waandishi wa habari ambao walitaka kufuatilia ziara ya waziri wa mambo ya nje Sergey Lavrov mjini New York, na Lavrov amesema kwamba Moscow itachukua hatua kali za ulipizaji kisasi.

Wizara ya mambo ya nje ya Marekani haikutoa mara moja maelezo juu ya madai ya kuwanyima visa wanahabari hao.

“Marekani inachukulia kwa uzito mkubwa wajibu wake kama nchi mwenyeji wa Umoja wa Mataifa kwa mujibu wa mkataba wa makao makuu ya Umoja wa Mataifa, ikiwemo kutoa visa,” msemaji wa wizara ya mambo ya nje alisema katika taarifa.

Wanahabari hao walikuwa na lengo la kufuatilia kuwepo kwa Lavrov kwenye jukwaa la Umoja wa mataifa kuashiria uenyekiti wa Russia kwenye Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa.

Akizungumza kabla ya kuondoka Moscow jana Jumapili, Lavrov alisema “ Nchi inayojiita yenye nguvu zaidi, yenye akili zaidi, huru na ya haki imejitokeza na kufanya jambo la kijinga kwa kuonyesha kile ambacho iliapa kuhusu kulinda uhuru wa kujieleza na kupata habari ni mambo muhimu.”

Amesema “muwe na uhakika kwamba hatutasahau na hatusamehe.”

XS
SM
MD
LG