Umoja wa Ulaya mwezi Mei ulitangaza kusitisha usambazaji wa kile ulichokitaja kuwa mitandao minne ya propaganda inayohusishwa na Kremlin, na kuondoa haki zao za utangazaji ndani ya umoja huo.
Ulisema wakati huo marufuku hiyo ililenga Sauti ya Ulaya, shirika la habari la RIA, na magazeti ya Izvestia na Rossiyskaya Gazeta.
Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia Jumanne imejibu kwa kutoa orodha ya vyombo 81 vya habari kutoka nchi 25 wanachama wa Umoja wa Ulaya, pamoja na vile vya Ulaya, ambavyo matangazo yake imesema hayatapatikana tena katika eneo la Russia.
Forum