Gavana wa eneo hilo Vitaly Kim kupitia ujumbe wa Telegram amesema kwamba mashambulizi hayo yalipiga katikati ya mji, na kwamba miongoni mwa waliojeruhiwa ni watoto watano, wakati watu wawili wakiokolewa kutoka kwenye vifusi.
Meya wa Mykolaiv, Oleksandr Snkevych, amesema kwamba shambulizi hilo limeharibu tarkriban majengo 5 ya ghorofa pamoja na maeneo mengine kadhaa ya kuegesha magari.
Na katika mji jirani wa Odesa, shambulizi la anga la Russia limemuua mtu mmoja. Russia imefanya mashambulizi kadhaa ya anga wiki hii dhidi ya Odesa na Mykolaiv, naye Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy alisema kupitia ujumbe wa Telegram kwamba “ Magaidi wa Russia wameendelea kuharibu maisha katika taifa letu .”
Wakati huo huo maafisa waliowekwa na Russia kwenye peninsula ya Crimea, wamesema kwamba drone ya Ukraine imeua mtu mmoja na kuharibu majengo kadhaa ya kiutawala kaskazini magharibi mwa peninsula hiyo.
Forum