Serhiy Lysak ambaye ni gavana wa Dnipropetrovsk amesema kwamba Russia imeharibu majengo matano ya makazi ya ghorofa wakati wa shambulizi hilo, na kwamba timu za waokozi zinaendelea kutafuta manusura.
Kryvyi Rih ndiyo mji alikozaliwa rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy wakati akiandika ujumbe wa Telegram na kusema kwamba Russia imeendelea kushambulia makazi na miji ya watu wa kawaida.
Ameongeza kusema kwamba magaidi hawatasamehewa kamwe, na kwamba watawajibishwa kwa kila shambulizi walilofanya. Shambulizi la Rih ni sehemu ya shambulizi la anga la Russia ambalo pia lililenga mji mkuu wa Kyiv pamoja na ule wa Kharkiv.
Wakari huo huo Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ameahidi kuendelea kutoa silaha pamoja na magari ya kivita kwa Ukraine katika wiki zijazo, akisema kwamba taifa lake lingependa kuona Ukraine ikiweza kujilinda kikamilifu dhidi ya Russia.
Forum