Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Oktoba 24, 2026 Local time: 23:39

Russia yafanya mashambulizi mapya ya anga Ukraine

Rusia ilizianzisha mashambulizi mapya ya anga nchini Ukraine Jumatatu, ikiwa ni mara ya tatu katika kipindi cha wiki moja, huku ikilenga mji mkuu wa Kyiv na miji mingine katika siku ya kwanza ya mwaka wa shule.

Shambulizi hilo kubwa lilitokea saa 11:30 alfajiri baada ya tahadhari ya anga ya nchi nzima, ingawa maafisa wa Ukraine wamesema idadi ya waliopoteza maisha ilikuwa ndogo na uharibifu wa mali ni mdogo.

Lakini shambulizi la Jumapili usiku kwenye kituo cha watoto yatima katika mji wa kaskazini mashariki wa Sumy lilijeruhi watoto wawili na watu wazima 11, kwa mujibu wa shirika la utangazaji la Ukraine, Suspilne.

Wakati huo huo, Ukraine imeishambulia Russia kwa kutumia ndege zisizo na rubani zilizolenga mitambo ya kufua umeme, ikiwa ni pamoja na moja karibu na Moscow, Jumapili ambayo ilisababisha moto na uharibifu mwingine.

This item is part of

Forum

​
XS
SM
MD
LG