Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 18:08

Russia yaanza kwa kishindo Kombe la Dunia


Wachezaji wa Russia wakishangilia ushindi wa 5 - 0 dhidi ya Saudi Arabia.
Wachezaji wa Russia wakishangilia ushindi wa 5 - 0 dhidi ya Saudi Arabia.

Russia wenyeji wa Kombe la Dunia Russia 2018 wameifunga Saudi Arabia mabao 5 - 0 katika mchezo wa ufunguzi wa kundi A, Alhamisi.

Rais wa Russia Vladmir Putin aliongoza mashabiki wa Russia katika mchezo huo uliofanyika katika uwanja wa Luzhniki mjini Moscow, uwanja wenye uwezo wa kuchukuwa watu elfu 80.

Timu ya Russia imeanza vizuri michuano hiyo kwa sasa kuongoza kwa muda kundi A ikiwa na pointi 3. Kwa sasa inasubiriwa mechi ya Ijumaa ya kundi hilo la A kati ya Misri ya Mohamed Salah na Uruguay ya Luis Suarez.

Kikosi cha Russia kabla ya mchezo wake dhidi ya Saudi Arabia
Kikosi cha Russia kabla ya mchezo wake dhidi ya Saudi Arabia

Mechi za makundi manane itaendelea hadi tarehe 28 Juni kabla ya kuanza mzunguko wa pili na mtoano utakaoanza Juni 30.

Magoli ya Russia yamefungwa na Yury Gazinsky (12), Denis Cheryshev (43 na 91) na Aleksandr Golovin (94).

Wengine waliokuwepo uwanjani leo hii kushuhudia mchezo huo ni rais wa FIFA Gianni Infantiono, na mwanamfalme wa Saudi Arabia, Mohammad Bin Salman Al Saud, ambaye alionekana kusononeka kwa kuona timu yake ikiadhibiwa na Russia.

Kikosi cha Saudi Arabia kabla ya mchezo wake na Russia
Kikosi cha Saudi Arabia kabla ya mchezo wake na Russia

Katika kudni A, kuna timu za Russia, Saudi Arabia, Uruguay, na Misri.

XS
SM
MD
LG