Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 07:52

Russia na Ukraine zatupiana shutuma za kuanzisha mashambulizi mapya karibu na kinu cha nyuklia


Zaporizhzhia Nuclear Power Plant near Enerhodar
Zaporizhzhia Nuclear Power Plant near Enerhodar

Russia na Ukraine siku ya Jumatano zilitupiana  shutuma za kuanzisha mashambulizi mapya karibu na kinu cha nyuklia kusini mwa Ukraine ambayo yameibua wasiwasi wa kimataifa kuhusu usalama kati kati ya mzozo

Madai hayo kutoka kwa pande hizo mbili ni ya hivi karibuni katika wiki za kunyoosheana vidole kuhusiana na mashambulizi karibu na kinu cha nyuklia cha Zaporizhzhia, na yanakuja wakati wakaguzi kutoka Umoja wa Mataifa wakielekea eneo hilo kufanya ukaguzi wa ulinzi na usalama.

Timu ya Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki iliondoka Kyiv leo Jumatano huku Mkurugenzi Mkuu wa IAEA Rafael Grossi akisema timu yake imepokea hakikisho kuwa itaweza kufanya kazi yao.

XS
SM
MD
LG