Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Machi 15, 2026 Local time: 15:08

Russia na Ukraine zabadilishana zaidi ya wafungwa 200 wa vita

Wafanyakazi wa jeshi la Russia walioachiliwa huru na Ukraine wakijianda kurejea Russia, Aprili 10, 2023
Wafanyakazi wa jeshi la Russia walioachiliwa huru na Ukraine wakijianda kurejea Russia, Aprili 10, 2023

Russia na Ukraine zimebadilishana zaidi ya wanajeshi 200 katika mabadilishano ya hivi karibuni ya wafungwa, maafisa wamesema Jumatatu.

Wizara ya ulinzi ya Russia imesema wanajeshi wake 196 waliachiliwa huru kutoka jela la Ukraine, naye Andriy Yermak, mkuu wa utawala kwenye ofisi ya Rais Volodymyr Zelenskiy amesema Russia iliwaachilia huru wafungwa 100 wa Ukraine.

Hakuna tangazo lililofichua maelezo ya jinsi ubadilishanaji wa wafungwa ulivyotekelezwa. Yermak amesema kwenye mtandao wa Telegram kwamba baadhi ya wanajeshi wa Ukraine wana majeraha mabaya na magonjwa.

Amesema ubadilishanaji wa wafungwa wa hivi karibuni katika vita vya miezi 14, “haukuwa rahisi”, lakini hakutoa ufafanuzi.

Ubadilishanaji wa wafungwa ni mojawapo ya mambo machache ambayo Ukraine na Russia zinashirikiana.

XS
SM
MD
LG