Wanajeshi wa Russia nao wameshambulia kusini mwa ukraine katika mji wa bandari Odesa kwa ndege zisizokuwa na rubani.
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy amesema kwamba karibu watu milioni 1.5 hawana umeme katika mkoa wa Odesa, ambako maafisa katika sehemu hizo wakiwasihi watu ambao nyumba zao zinategemea umeme pekee, kuondoka.
Maafisa wamesema kwamba inaweza kuwachukua wiki au miezi kadhaa kukarabati mfumo wa umeme ambao umeharibiwa na makombora ya Russia katika eneo hilo.
Makombora 15 ya ndege zisizokuwa na rubani yameangushwa Odesa na sehemu zilizo karibu, huku makombora 10 yakinaswa na mifumo ya Ukraine.
Ofisi ya mwendesha mashtaka wa Ukraine imesema kwamba makombora yaliyorushwa na wanajeshi wa Russia yametengenezwa nchini Iran.