Russia imesema mapema Ijumaa kwamba imetungua ndege kadhaa zisizokuwa na rubani zilizorushwa kutoka Ukraine.
Wizara ya ulinzi ya Russia imesema ndege 42 zisizo na rubani ziliharibiwa katika eneo la Crimea, tisa zilitunguliwa na vikosi vya ulinzi wa anga, 33 kwa mfumo wa kielektroniki wa vita.
Crimea ilitekwa na Russia mwaka 2014. Hakuna taarifa za haraka za vifo. Wizara ya ulinzi ya Marekani imesema Alhamisi kwamba itatoa mafunzo kwa raia wa Ukraine kurusha na kuendelea kuziboresha ndege za kivita aina ya F-16.
Wizara ya Ulinzi imesema katika taarifa yake kwamba mafunzo hayo yatafanyika katika kambi ya ulinzi wa taifa ya Morris Air huko Tucson, kwenye jimbo la Arizona nchini Marekani na yatasimamiwa na kikosi cha ulinzi wa taifa cha 162.
Forum