Katika taarifa zake za kijasusi za kila siku kuhusu Ukraine wizara ya ulinzi ya Uingereza ilisema Jumamosi kwamba Russia inajitahidi kudumisha uthabiti wa maelezo yake ya msingi inayoyatumia kuhalalisha vita nchini Ukraine.
Maelezo ni kwamba uvamizi kwa Ukraine ni sawa na uzoefu wa Sovieti katika Vita Kuu ya Pili ya Dunia. Mapema mwezi huu Russia ilielezea masuala ya usalama kama sababu ya kufuta maadhimisho ya kila mwaka ya maandamano ya kumbukumbu ya Kikosi kisichosahaulika cha Vita Kuu ya Uzalendo-Great Patriotic War.
Kiuhalisia wizara ilisema, mamlaka ilikuwa na wasiwasi mkubwa kwamba washiriki wangeangazia suala la hasara kubwa ya karibuni waliyoipata warussia. Kwa upande mwingine ya maelezo ya Russia ni kilio cha maandamano kwamba kuna Wa-nazi nchini Ukraine. Lakini hivi sasa, hata hivyo, Yevgeny Prigozhin, ambaye ni mkuu wa Kundi la Wagner na pia rafiki wa Rais wa Russia, Vladimir Putin, amehoji hadharani uwepo wa Wa-nazi nchini Ukraine inapingana na uhalali wa Russia kwa uvamizi huo wizara ya Uingereza imesema.
Katika hotuba yake kwa njia ya video Ijumaa usiku, Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy alisema Ukraine iko tayari kwa ajili ya kukabiliana na mashambulizi.