Shirika hilo lilisema habari za kuunganishwa huko zinatokana na ripoti ya Tass kwamba mikoa ya Donetsk na Luhansk na mikoa ya Zaporizhzhia na Kherson imewekwa chini ya usimamizi wa kamandi ya kijeshi ya nyota tatu iliyoko Rostov-on-Do.
Ripoti hiyo ilisema, hata hivyo, hatua hiyo haina uwezekano wa kuwa na athari za haraka katika uvamizi wa Russia nchini Ukraine.
Kundi la Nchi Saba zilizoendelea kiviwanda duniani zilikubaliana Ijumaa juu ya kukomo wa bei ya usafirishaji wa mafuta yaliyosafishwa ya Russia.
Waziri wa Fedha wa Marekani Janet Yellen alisema katika taarifa yake kwamba makubaliano hayo yanafuata kikomo sawa cha bei kwa mauzo ya mafuta ghafi ya Russia kilichowekwa mwezi Desemba na kusaidia kuendeleza malengo yao ya kuzuia kitu kikuu kinachoingiza mapato ya Russia katika kufadhili vita vyake haramu nchini Ukraine.
Facebook Forum