Gazeti hilo limesema kwamba mkuu wa jeshi la Ukraine ameripoti kwamba wanajeshi 346,070 wamekufa wakiwemo 1,250 waliokufa ndani ya saa 24 zilizopita.
Ripoti zimeongeza kusema kwamba Russia imepoteza vifaru 5,739, magari ya kivita 10,692, magari ya kawaida 10,766 pamoja na yale ya kubeba mafuta, mizinga 8,137, mifumo 923 ya kurushia makombora, mifumo 609 ya ulinzi wa anga, ndege 324 za kivita, helikopta 324, droni 6,278 na meli 22 pamoja na boti na manowari kadhaa.
Wakati huo huo wizara ya Ulinzi ya Uingereza imetoa maoni yake kuhusu tangazo la Russia la mwezi huu kwamba mikoa kadhaa ya Ukraine ikiwemo Donetsk, Luhansk, Kherson na Zaporizhzhia itashiriki kwenye uchaguzi wa rais uliopangwa kufanyika mwezi Machi mwakani. Mikoa hiyo pia ilijumuishwa kwenye uchaguzi wa majimbo uliyofanyika Septemba.
Forum