Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 09:43

Russia imeonya Marekani kuhusiana na msaada wake wa silaha kwa Ukraine


Msaada wa silaha kwa Ukraine kutoka kwa serikali ya Marekani ukipakuliwa kutoka kwa ndege katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Boryspil, nje ya mji wa Kyiv, Ukraine Feb 13, 2022
Msaada wa silaha kwa Ukraine kutoka kwa serikali ya Marekani ukipakuliwa kutoka kwa ndege katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Boryspil, nje ya mji wa Kyiv, Ukraine Feb 13, 2022

Wizara ya mambo ya nje ya Russia imeonya Marekani kwamba iwapo itapelekea Ukraine silaha za kisasa za kulinda anga yake, utawala wa Moscow itachukulia hatua hiyo kama ya uchokozi na italazimisha Russia Kujibu.

Msemaji wa wizara ya nje ya Russia Maria Zakharova, amesema kwamba hatua ya Marekani kupeleka makombora ya kujilinda kunasa makombora ya Russia ni hatua ya Marekani kujiingiza zaidi katika mgogoro huo na ya kusaidia Ukraine katika vita hivyo ambavyo zimeingia mwezi wa kumi.

Russia imeonya kwamba hatua hiyo itakuwa na athari zake.

Zakharova hajasema hatua zitakazochukuliwa na Moscow, lakini amesema kwamba Marekani inastahili kuthathmini hatua yake kutokana na onyo la Russia kwamba silaha zinazotolewa na Marekani kwa Ukraine zinalenga mashambulizi yanayotekelezwa na Russia.

Amesema kwamba Marekani sasa imekuwa sehemu ya moja kwa moja katika vita hivyo.

Tayari Marekani imetoa mafunzo kwa karibu wanajeshi 3,100 wa Ukraine, namna ya kutumia silaha hizo.

XS
SM
MD
LG