Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Oktoba 03, 2024 Local time: 14:41

Russia ilirusha ndege isiyokuwa na rubani nchini Ukraine


Mfano wa ndege isiyotumia rubani yaani drone
Mfano wa ndege isiyotumia rubani yaani drone

Maeneo yaliyolengwa ni pamoja na Kyiv, mji mkuu, na mkoa wa kusini wa Kherson na mkoa wa magharibi wa Khmelnytsky. “Ndege zisizo na rubani zilishambulia kwa makundi, katika mawimbi, na kutoka pande tofauti”, alisema Shehiy Popko mkuu wa utawala wa kijeshi wa Kyiv

Russia ilirusha ndege isiyokuwa na rubani nchini Ukraine leo Jumamosi. Jeshi la anga la Ukraine limesema vikosi vyake na makundi madogo yanayoangazia ndege zisizotumia rubani yaliangusha ndege 30 kati ya 31 aina ya Shehed zisizotumia rubani za Iran wakilenga maeneo 11 ya Ukraine.

Maeneo yaliyolengwa ni pamoja na Kyiv, mji mkuu, na mkoa wa kusini wa Kherson na mkoa wa magharibi wa Khmelnytsky. “Ndege zisizo na rubani zilishambulia kwa makundi, katika mawimbi, na kutoka pande tofauti”, alisema Shehiy Popko mkuu wa utawala wa kijeshi wa Kyiv.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky. October 8, 2023.
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky. October 8, 2023.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy alisema katika hotuba yake ya kila siku kwamba alifanya mkutano wa Bunge ya Mamlaka Serikali za Mitaa na Mikoa huko Lyiv Ijumaa. Maafisa wa serikali ya kitaifa, akiwemo Waziri Mkuu pia walihudhuria, kwa mujibu wa Zelenskyy.

Forum

XS
SM
MD
LG