Timu yote ya Russia ya wachezaji wenye ulemavu siku ya Jumapili ilipigwa marufuku kushiriki katika mashindano ya mwezi Septemba.
Hatua hiyo ni adhabu kwa nchi hiyo, yenye mpango maalum ya utumiaji wa dawa za kusisimua misuli, ambayo imezidi ile adhabu iliyotolewa kwa wanariadha waliotaka kushindana kwenye mashindano ya olimpiki ya msimu wa kiangazi yanayoendelea sasa hivi mjini Rio De Janeiro, Brazil.
Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki, IOC, ilikubali wanariadha wapatao 271 kutoka Russia kushiriki katika michezo ya Rio, ambayo ni asili mia 70 ya timu iliyoyotaka kushiriki hapo awali.
Hata hivyo, kamati ya kimataifa ya mashindano ya walemavu ililaani mpango wa Russia wa kukabiliana na dawa za kusisimua misuli, ikiwa ni pamoja na wanariadha walioshiriki kwenye mashindano ya Sochi yam waka wa 2014, na kuwapiga marufuku wanariadha wote wa nchi hiyo waliotarajia kushiriki katika mashindano ya Olimpiki ya Septemba 7 hadi 18 yatakayofanyika mjini Rio vile vile.