Rusesabagina alikuwa aznatumikia kifungo nchini Rwanda baada ya kukutwa na hatia kwa makosa aliyoshtakiwa.
Ndege iliyombebaa Rusesabagina, iliwasili Houston jumatano adhuhuri, kabla ya kuelekea katika hospitali ya kijeshi katika mji wa San Antonio.
Rusesabagina, mwenye umri wa miaka 68, mkaazi wa kudumu wa Marekani, raia w Ubelgiji, alituzwa na kusifiwa kwa kuwapa hifadhi zaidi ya watu 1,000 kutoka kabila la Watutsi wakati wa mauaji ya kimbari yam waka 1994 nchini Rwanda ambapo zaidi ya watu 800,000 waaliuawa.
Alitoweka mnamo mwaka 2020 alipokuwa ameitembelea Dubai huko umoja wa falme za kiarabu, nasiku chache baadaye alijikuta nchini Rwanda. Iliripotiwa kwamba alitekwa nyara na maafisa wa serikali ya Rwanda.
Alihukumiwa kifungo cha miaka 25 gerezani nchini Rwanda mwaka 2021 baada ya kukutwa na hatia kwa makossa nane yakiwemo kuwa mwanachama wa kundi la kigaidi, mauaji na utekaji nyara.
Serikali ya Rwanda ilimshutumu Rusesabagina kwa kuliunga mkono kundi lenye silaha linalopinga utawala wa rais Paul Kagame la Rwandan movement for democratic change RMDC.
Kundi hili lilidai kutekeleza mashambulizi yam waka 2018 na 2019 kusini mw Rwanda, ambapo watu tisa waliuawa.
Alitoa ushahidi mahakamani kwamba alilisaidia kuunda kundi hilo kuwasaidia wakimbizi na wala siyo kusababisha vurugu, na alijitenga na mashambulizi yaliyofanywa na kundi hilo.
Alisema kwamba alikamatwa kwa kuwa mkosoaji wa muda mrefu wa rais Paul Kagame kwa ukandamizaji wa haki za binadamu. Serikali ya Kagame imekuwa ikikanusha shutuma dhidi yake kwa ukandamizaji wa haki za kibinadamu na maujai ya raia wa Rwanda.
Rusesabagia aliandika barua kwa rais Paul Kagame ambayo ilichapishwa na wizara ya sheria ya Rwanda, akisema kwamba iwapo atasamehewa na kuachiliwa kurudi Marekani, hatajihusisha kabisa na siasa za Rwanda wala kumkosoa rais Paul Kagame.