Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Julai 22, 2024 Local time: 18:04

Rudy Giuliani huwenda akateuliwa waziri wa mambo ya nje


Rudy Giuliani, meya wa zamani wa mji wa New York.
Rudy Giuliani, meya wa zamani wa mji wa New York.

Wakati rais mteule wa Marekani Donald Trump akiendendelea kupanga serikali yake mpya vyanzo karibu naye vinaeleza kuwa aliekuwa meya wa mji wa New York, Rudy Giuliani huenda akateuliwa kuwa waziri wa mambo ya nje wa Marekani.

Giuliani ameshawahi kuwa muongoza mashitaka wa serikali lakini hana uzoefu wa sera za kigeni swala ambalo ni muhimu kwa wale wanaochukua wadhifa huo. Waziri wa mambo ya nje wa Marekani aliyeko madarakani John Kerry aliwahi kuwa mwenyekiti wa kamati ya senate ya uhusiano wa kimataifa kabla ya kuwa waziri wa mambo ya nje.

Condoleeza Rice aliyemtangulia alikuwa mshauri mkuu wa maswala ya usalama wa Rais George W. Bush. Colin Powell alikuwa mshauri wa kitaifa na pia mkuu wa majeshi huku Madeleine Albright akiwa mjumbe maalum wa Marekani kwenye Umoja wa Mataifa kabla ya kuwa waziri. Lakini Guliani alikuwa muungaji mkono mkuu wa Trump wakati wa kampeni na wamekuwa marafiki wa karibu kwa muda mrefu.

XS
SM
MD
LG