Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 13:12

Ronaldo atajwa kuweka historia nyingine katika malipo ya soka


Mchezaji wa soka wa Ureno Cristiano Ronaldo akiwa ameshikilia shati ya klabu ya Al-Nassr ya Saudia Arabia baada ya kusaini mkataba wa kihistoria katika soka la Mashariki ya Kati. REUTERS.
Mchezaji wa soka wa Ureno Cristiano Ronaldo akiwa ameshikilia shati ya klabu ya Al-Nassr ya Saudia Arabia baada ya kusaini mkataba wa kihistoria katika soka la Mashariki ya Kati. REUTERS.

Christiano Ronaldo alikamilisha uhamisho wa malipo ya kiwango cha  juu kwa kujiunga na  klabu ya Al Nassr ya Saudi Arabia siku ya Ijumaa katika mkataba ambao ni wa kihistoria katika soka la Mashariki ya Kati.

Christiano Ronaldo alikamilisha uhamisho wa malipo ya kiwango cha juu kujiunga na klabu ya Al Nassr ya Saudi Arabia siku ya Ijumaa katika mkataba ambao ni wa kihistoria katika soka la Mashariki ya Kati lakini utamshuhudia mmoja wa nyota wakubwa barani Ulaya akitoweka kutoka kwenye michuano ya viwango vya juu vya mchezo huo.

Al Nassr ilichapisha picha kwenye mitandao ya kijamii ya mshindi huyo wa Ballon d’or mara tano akiwa ameshikilia jezi ya timu hiyo baada ya Ronaldo kusaini mkataba hadi Juni 2025, huku klabu hiyo ikisifu uhamisho huo kuwa ni historia inayoandikwa.

"Huu ni usajili ambao hautaitia msukumo klabu yetu tu kupata mafanikio makubwa zaidi bali pia utatia msukumo kwenye ligi yetu, taifa letu na vizazi vijavyo, wavulana na wasichana kuwa bora zaidi klabu hiyo iliandika.

Pia inampa Ronaldo mwenye umri wa miaka 37 malipo makubwa zaidi ambayo yanaweza kuwa mkataba wa mwisho wa maisha yake ya soka. Vyombo vya habari vimedai kuwa nyota huyo wa Ureno anaweza kupata hadi dola milioni 200 kwa mwaka kutokana na mkataba huo, jambo ambalo litamfanya kuwa mchezaji wa soka anayelipwa pesa nyingi zaidi katika historia.

XS
SM
MD
LG