Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 20, 2024 Local time: 05:30

Ronaldo aongoza timu yake mpya katika ushindi


Mchezaji Cristiano Ronaldo akiwa ameshikilia jezi ya klabu yake mpya Al-Nassr ya Saudi Arabia baada ya kusaini mkataba utakaodumu hadi 2025.REUTERS
Mchezaji Cristiano Ronaldo akiwa ameshikilia jezi ya klabu yake mpya Al-Nassr ya Saudi Arabia baada ya kusaini mkataba utakaodumu hadi 2025.REUTERS

Mchezaji mkongwe Cristiano Ronaldo alicheza mechi yake ya kwanza ya kiushindani katika klabu yake mpya ya Al Nassr katika mechi waliyopata ushindi wao wa bao  1-0 dhidi ya Ettifaq kwenye Ligi ya Saudia Jumapili.

Mshambuliaji huyo wa Ureno mwenye umri wa miaka 37 alijiunga na klabu hiyo mwezi uliopita kwa mkataba utakaodumu hadi 2025, akiripotiwa kulipwa zaidi ya paundi milioni 177 kwa mwaka.

Aliongoza na kucheza mechi nzima ambapo kiungo wa Brazil Anderson Souza Conceição, au Talisca alifunga bao la ushindi.

Al Nassr wako kileleni mwa ligi ya Saudia Arabia wakiwa na pointi moja juu ya Al Hilal iliyo nafasi ya pili.

Ronaldo ambaye aliwahi kuzichezea Manchester United, Juventus na Real Madrid alilakiwa na mabango na shangwe kutoka kwa mashabiki wake na wapenzi kwenye Uwanja wa Chuo Kikuu cha King Saud mjini Riyadh.

XS
SM
MD
LG