Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Mei 31, 2024 Local time: 01:15

Ron DeSantis kutangaza kugombea urais 2024 Marekani akiwa na Musk kupitia Twitter


FILE- In this March 5, 2019 file photo, Florida Gov. Ron Desantis gives his state of the state address on the first day of the legislative session in Tallahassee, Fla. De Santis has pushed for a repeal to Florida's ban on smokable medical marijuana…
FILE- In this March 5, 2019 file photo, Florida Gov. Ron Desantis gives his state of the state address on the first day of the legislative session in Tallahassee, Fla. De Santis has pushed for a repeal to Florida's ban on smokable medical marijuana…

Gavana wa Florida Ron DeSantis Jumatano anatarajiwa kutoa tangazo ambalo limesubiriwa  kwa muda mrefu la kugombea urais mwaka 2024  kwa mtindo usio wa kawaida katika tukio na bilionea Elon Musk kwenye mtandao wa Twitter.

FILE PHOTO: Elon Musk
FILE PHOTO: Elon Musk

Kuingia kwake katika kinyang’anyiro cha urais kunabadilisha mwelekeo wa ushindani kuwania uteuzi wa Republican, kwa kuwa kuna uwezekano ataibuka kuwa mpinzani mkubwa sana wa rais wa zamani Donald Trump . Mgombea atakayeteuliwa atachuana na Rais Joe Biden , mdemocrat katika uchaguzi mkuu wa Novemba mwaka kesho.

DeSantis mwenye umri wa miaka 44 pia anapanga kuwasilisha nyaraka katika tume ya uchaguzi akitangaza rasmi ugombea wake, wafanyakazi wake wamesema.

Musk, mkurugenzi mkuu wa Tesla na Twitter akiwa na wafuasi milioni 140 katika twitter amesema kutokea kwake katika tukio hilo sio kumuidhinisha lakini litaonyesha nia yake ya kufanya utaratibu huo kuwa sawia zaidi.

Leo pia Desantis atafanya Mkutano na wachangiaji wake wakubwa katika hoteli ya Miami, ambako watazindua rasmi juhudi zake za uchangishaji.

Forum

XS
SM
MD
LG