Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Septemba 26, 2022 Local time: 13:17

Romney amteua mhafidhina kuwa mgombea mwenza


Mbunge Paul Ryan, akimkaribisha gavana wa zamani wa Massachusetts Mitt Romney mjini Milwaukee, Wisconsin, Aprili 3, 2012.

Mgombea kiti cha rais kwa niaba ya chama cha Republican cha Marekani, amteua Paul Rayn kuwa mgombea mwenza kwa ajili ya uchaguzi wa Novemba

Mitt Romney alitoa tangazo hilo Jumamosi asubuhi mbele ya wafuasi wake juu ya manuari ya kijeshi isiyo vitani tena ya USS Wisconsin mjini Norfolk katika jimbo la Virginia.

Rayn mwenye umri wa miaka 42 ni mbunge wa muda mrefu kutoka jimbo la Wissconsin anaeungwa mkono na wahafidhina wenye ushawishi mkubwa wanaotetea mageuzi katika chama cha Republican.

Mgombea mwenza huyo ni mwenyekiti wa kamati ya bajeti ya baraza la wawakilishi katika bunge la Marekani, na ni mbunge aneongoza juhudi za kupunguza nakisi katika bajeti ya Marekani.

Romney akijitokeza pamoja na Rayn huko Norfolk kuanza kampeni ya siku nne ya kuzunguka kwa basi.
XS
SM
MD
LG