Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Juni 18, 2024 Local time: 11:37

Rolene Strauss apewa Taji la Mrembo wa Dunia


Picha ya mrembo wa dunia Rolene Strauss
Picha ya mrembo wa dunia Rolene Strauss

Mwanamke wa miaka 22 kutoka Afrika Kusini ameshinda Taji la Mrembo wa Dunia, wakati wa mashindano ya 64 ya yanayofanyika kila mwaka. Rolene Strauss mwanafunzi alivishwa taji hilo Jumapili jijini London.

Mamilioni ya watu kote duniani walitazama sherehe hizo kupitia televisheni. Edina Kulscar wa Hungary alichukua nafasi ya pili na M’marekani Elizabeth Safrit akichukua nafasi ya tatu.

Kutoka bara la Afrika mrembo pekee aliyeingia katika kundi la warembo kumi bora kwenye ushindani huo mkali ni Mkenya Idah Nguma. Zaidi ya nchi 120 ziliwakilishwa kwenye mashindano hayo.

Mashindano ya mwaka huu ya kutafuta mrembo wa dunia yaligubikwa na mkasa pale mrembo Maria Jose Alvarado kutoka Honduras ambaye alikuwa kwenye mashindano hayo alipouawa pamoja na dadake mwezi jana. Polisi wanamtuhumu mpenzi wa dadake katika mauaji hayo.

Mshindi mpya wa Taji la Mrembo wa Dunia amesema anapanga kwenda Honduras kusaidia ujenzi wa shule kwa heshima ya dada hao wawili waliouawa.

XS
SM
MD
LG