Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Juni 23, 2024 Local time: 08:30

Robo Fainali ya UEFA Euro 2016 Kuanza Weekend Hii


Mechi za soka za robo fainali ya UEFA EURO 2016 zinatarajiwa kuanza weekend hii huku mchezo wa kusisimua jumamosi hii ukitarajiwa kuwa kati ya Croatia yenye viungo mahiri na Ureno inayoongozwa na mchezaji mahiri kabisa wa ulimwengu Cristiano Ronaldo.

Katika mechi nyingine za mashindano hayo, Uswisi inatajiwa kuteremka dimbani kuumana na Poland wakati Wales inayomtarajia sana mshambuliaji wake mahiri na wa Real Madrid ya Hispania Gareth Bale ikitarajiwa kuvuka kisiki kigumu cha Ireland ya kaskazini.

Croatia, timu inayotabiriwa kuonyesha maajabu katika mashindano haya ina matarajio makubwa ya kuwarudisha nyumbani Cristiano Ronaldo na Ureno ingawa wachambuzi wanasema haitoweza kuwa kazi rahisi haswa ukizingatia kiwango kilichoonyeshwa na mchezaji huyo katika mechi ya mwisho dhidi ya Hungary.

UEFA EURO 2016
UEFA EURO 2016

​Wenyeji wa mashindano hayo Ufaransa watashuka dimbani jumapili kwenye mchuano mkali dhidi ya Jamhuri ya Ireland huku Ujerumani wakitarajiwa kuwa na mechi rahisi dhidi ya Slovakia. Ubelgiji, timu iliyotabiriwa pia kufanya makubwa itakuwa katika mji wa Toulouse ikigombea tiketi ya nusu fainali dhidi ya Hungary.

Mchezaji kiungo wa Ufaransa Dimitri Payet ambaye mpaka sasa ameushangaza ulimwengu wa soka kwa kuonyesha kiwango cha hali ya juu ni mmoja wa wachezaji wanaotarajiwa kufanya makubwa zaidi katika michuano ya robo fainali na amekuwa tegemeo kubwa la Ufaransa kwa sasa tofauti na ilivyotarajiwa mwanzoni. Kiungo huyo wa timu ya West Ham ya Uingereza ambaye mpaka sasa amekuwa akitarajiwa kusajiliwa na timu kubwa za soka barani ulaya amesisitiza kuwa ataendelea kubaki kwenye timu yake ya West Ham msimu ujao.

XS
SM
MD
LG