Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, uhaba mkubwa sana uko kwenye dawa zinazotumika kwa matibabu ya saratani wakati zaidi ya taasisi 1,123 zilizohojiwa zilisema kwamba zimelazimika kuweka viwango vya matumizi kwa matibabu kama hayo.
Utafiti huo ilifanyika kati ya Juni 23 na Julai 14 na taasisi hiyo ya ASHP ambayo inawakilisha zaidi ya wauza dawa na wafamasia 60,000 kote nchini. Kulingana na utafiti huo, ingawa mahitaji ya juu ya dawa kama zile za kisukari za Ozempic, ambayo husababisha uhaba wa muda mfupi, ambapo uhaba mkubwa unaoendelea unasukumwa na vigezo vya uchumi ikiwa ni pamoja na ushindani wa bei miongono mwa watengeneza dawa.
Mkurugenzi mkuu wa ASHP Paul Abramowitz amesema kwamba kwa baadhi ya kesi hakuna namna ya kupata mbadala wa dawa zenye uhaba, suala linalowaweka wagonjwa kwenye hatari.
Ameongeza kusema kwamba bunge linahitaji kushughulikia uhaba uliopo. Mwezi Juni idara ya Marekani inayosimamia ubora wa chakula na dawa FDA ilisema kwamba inatafuta vyanzo vipya vya dawa ili kupunguza uhaba wa dawa kama vile methotrexate inayotumiwa kwenye matibabu ya saratani, wakati pia ikijitahidi kupunguza uhaba wa dawa za matibabu ya chemotherapy.
Forum