Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Juni 13, 2025 Local time: 13:41

Ripoti China na Cuba zimefikia makubaliano muhimu; Pentagon inasema sio sahihi


Msemaji wa Pentagon Brigedia Jenerali Pat Ryder. Washington, Feb. 10, 2023.
Msemaji wa Pentagon Brigedia Jenerali Pat Ryder. Washington, Feb. 10, 2023.

"Naweza kukuambia kwa kuzingatia taarifa tulizonazo, kwamba hiyo sio sahihi. Kwamba hatujui China na Cuba wanajenga aina yoyote ya kituo cha ujasusi", msemaji wa Pentagon, Brigedia Jenerali Pat Ryder aliwaambia waandishi wa habari akiwa Pentagon siku ya Alhamisi

Wizara ya ulinzi ya Marekani-Pentagon inasema ripoti kwamba China na Cuba zimefikia makubaliano ya siri yanayoruhusu Beijing kujenga kituo kinachonasa mawasiliano kielektroniki katika kisiwa hicho ambacho kiko umbali wa kilomita 160 kutoka Marekani sio sahihi.

"Naweza kukuambia kwa kuzingatia taarifa tulizonazo, kwamba hiyo sio sahihi. Kwamba hatujui China na Cuba wanajenga aina yoyote ya kituo cha ujasusi" msemaji wa Pentagon, Brigedia Jenerali Pat Ryder aliwaambia waandishi wa habari akiwa Pentagon siku ya Alhamisi.

Kwa mujibu wa ripoti hizo ambazo zilionekana kwa mara ya kwanza katika jarida la Wall Street likinukuu maafisa wa ujasusi ambao hawakutajwa majina, China imekubali kuilipa Cuba dola bilioni kadhaa kwa ajili ya kituo hicho cha ujasusi, ambacho kitaiwezesha China kukusanya mawasiliano ya kielektroniki kutoka kusini mashariki mwa Marekani, mahala ambako kambi nyingi za kijeshi ziko huko.

Forum

XS
SM
MD
LG