Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Septemba 19, 2024 Local time: 14:59

Machar kushika tena wadhifa wa makam rais, Sudan Kusini


Kiongozi wa waasi Riek Machar akihutubia kikao mjini Kampala,Uganda, Januari mwaka huu.
Kiongozi wa waasi Riek Machar akihutubia kikao mjini Kampala,Uganda, Januari mwaka huu.

Kiongozi wa upinzani wa Sudan Kusini Riek Machar amemhakikishia katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa kuwa yuko tayari kuchukua wadhifa wake tena kama makamu wa rais.

Kiongozi wa waasi wa Sudan Kusini Riek Machar amemhakikishia katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon, kuwa yuko tayari kurejea kwenye mji mkuu wa Juba mwezi Machi kuchukua wadhifa wake tena, kama makamu wa rais wa Sudan Kusini.

Kwenye mahojiano na VOA, Bw. Machar amesema kuwa , anacho subiri ni awamu ya kwanza ya mipango ya kiusalama kama ilivyo kubaliwa kwenye mkataba wa amani.

Katibu huyo wa Umoja wa Mataifa alitaka hakikisho kutoka kwa Machar kwamba ataelekea Juba kuapishwa kuwa makamu wa rais katika harakati ya kuunda serikali ya muungano ya mpito , hatua inayonuia kumaliza ghasia na kuleta amani kwenye taifa hilo changa zaidi ulimwenguni.

Machar amesema kuwa Ban Ki Moon ameahidi kuunga mkono utekelezaji wa mkataba huo aliotia saini na Rais Salva Kiir. Matamshi yake yamekuja baada ya kiongozi huyo wa Umoja wa Mataifa kukutana na rais Kiir siku ya Alhamisi.

XS
SM
MD
LG