Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Juni 19, 2024 Local time: 19:33

REG ya Rwanda wapata ushindi dhidi ya SLAC


Mamadi Keita (S.L.A.C.), BAL President Amadou Gallo Fall and Abel Abdourahmane Diop (DUC) at BAL 2022 opening game in Dakar, Senegal.
Mamadi Keita (S.L.A.C.), BAL President Amadou Gallo Fall and Abel Abdourahmane Diop (DUC) at BAL 2022 opening game in Dakar, Senegal.

Timu ya REG ya Rwanda (REG) ilipata ushindi mwingine  mwembamba dhidi ya timu ya Seydou Legacy Athletique Club (SLAC) ya Guinea, kwa jumla ya pointi  83 kwa 81.

Anthony miller Jr. wa SLAC anapachika kikapu cha pointi mbili wakati mchezo ukiendelea katika robo ya kwanza.

Mbaye alitumbukiza mpira wavuni kwa mkono mmoja kupunguza uongozi wa SLAC hadi pointi mbili.

Elie Kaje wa Rwanda anatoa asisti kwa Walker ambaye alipachika pointi mbili na kufikisha mchezo sare mpaka mapumziko.

Nshobozwa wa REG anampasia Thomas jr anayepachika pointi mbili na kudumisha uongozi wao .

Nshobozwa tena anafanya vitu vyake kwa kutoa asisti nyingine kwa Thomas Jr. na kuwa sare tena mwishoni mwa kota ya 3.

Zikiwa zimesalia dakika tatu kabla ya mchezo kumalizika, Thomas jr anafunga pointi tatu, na kuendeleza uongozi wa Rwanda hadi pointi 4.

Zikiwa zimesalia sekunde 16 pekee REG wanapoteza mpira kwa SLAC, huku Obekpa akikimbia uwanjani na kumpasia Fofana ambaye anarudisha kwa Obekpa na alifunga na kuwaweka mbele kwa pointi moja.

Ikiwa kumebaki sekunde chache nne tu Thomas Jr alimpatia pasi Nshobozwa ambaye alipachika pointi 3 na kuitoa Rwanda kimaso maso kushinda mchezo huu wa pili kwa timu hii.

XS
SM
MD
LG