Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 12:14

Dunia yaadhimisha siku ya wakimbizi Juni 20


Watoto wa kiiraqi walotoroka vita wakiwa kwenye kambi ya wakimbizi ya al-Hawl takriban kilomita kutoka mpaka na Syria
Watoto wa kiiraqi walotoroka vita wakiwa kwenye kambi ya wakimbizi ya al-Hawl takriban kilomita kutoka mpaka na Syria

June 20 ni siku ya wakimbizi duniani.

Mara kadhaa wakimbizi huacha kila kitu chao nyuma wakikimbia maeneo yenye mizozo .

Watetezi wa haki za binadamu wanasema wakimbizi ni wajasiri, lakini sehemu muhimu ya safari yao inakuja wakati inapowalazimu kuzoea makazi yao mapya.

Naibu mkuu wa masuala ya nje katika taasisi ya maendeleo Marekani, American Progress, Bi Winnie Stachelberg, anasema kupata makazi mapya kwa wakimbizi ni suala umhimu duniani na kuna haja ya kupatiwa suluhisho la kudumu.

Anasema huu sio wakati wa kurudi nyuma, lakini ni nafasi ya kuongoza kwa kuonyesha mfano.

Katika miji kama vile Fargo jimbo la North Dakota linafanya hivyo.

Kwa mujib wa meya wa jimbo hilo Tim Mahoney, jamii inaungana kuwasaidia wakimbizi kupata ahuweni na kuanza kujenga maisha mapya.

Anasema mji wao unakuwa, uchumi uko mzuri na mambo mazuri yanafanyika hapo.

Mahoney anasema takriban kila mwaka wakimbizi mia 5 wanahamia Fargo.

Mahoney anasema wakimbizi wanaleta mambo mengi mazuri kwa mji huo kama vile tamaduni mpya, chakula na dini.

Mkimbizi Vicky Xiong,kushotoakimfundisha mwanawe, Rachel Lor kufuma nyumbani mwao huko Fresno, California. Vicky na mwanawe ni wakimbizi kutoka Laos, wanaoishi Marekani.
Mkimbizi Vicky Xiong,kushotoakimfundisha mwanawe, Rachel Lor kufuma nyumbani mwao huko Fresno, California. Vicky na mwanawe ni wakimbizi kutoka Laos, wanaoishi Marekani.

Bi Susan Khozouri naibu mkuu wa idara ya kuwatafutia makazi wakimbizi ya HIAS anasema, pale wakimbizi wanapowasili hapa serikali ya Marekani tayari imeshatambua kuwa watu hawa wanahitaji msaada wa kibinadamu kutoka Marekani, na watakuwa na haki ya kufanya kazi na kuishi katika muda wa mwaka mmoja tangu wanapowasili kuweza kupata uraia wa Marekani baada ya miaka 5 iwapo watapendelea.

Kulingana na idara ya wakimbizi ya umoja mataifa UNHCR, kuna takriban wakimbizi millioni 60 waliopoteza makazi yao kote duniani, wengi wao kutoka nchi za Syria, Afghanistan, Somalia na Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo.

Serikali ya rais Obama inapanga kuwaingiza wakimbizi kutoka Syria takriban elfu 10 katika mwaka wa fedha wa 2016, kama mpangilio wa lengo jumla la kuwaingiza wakimbizi takriban elfu 85 kutoka kote duniani.

XS
SM
MD
LG