Shambulizi hilo la Ijumaa jioni limefanyika kwenye mji wa Vugizo karibu na mpaka wa Jamhuri ya Kidemokrais ya Congo, ambao ni ngome ya kundi hilo. Serikali imeongeza kusema kwamba shambulizi hilo la 'kigaidi na la kikatili,' lililenga raia, wakati likiua watoto 12, wakiwemo watano waliyopo chini ya umri wa miaka 5, wanawake watatu wakiwawemo wawili wajawazito na wanaume watano akiwemo polisi mmoja aliyekuja kuwasidia.
Watu wengine 9 wajeruhiwa wakati wakiendelea kupokea matibabu hospitalini. Kundi la RED- Tabara kupitia ujumbe wa X iliyojulikana awali kama Twitter, limesema kwamba wapiganaji wake waliyopo Burundi wameshambulia kituo cha mpakani cha Vugizo, na kwamba wanajeshi 9 na polisi mmoja wameuliwa. Vyanzo viwili vya kijsehi na kiusalama vimeambia shirika la habari la AFP kwamba shambulizi hilo lililenga kituo cha kijeshi
Forum