Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 04, 2022 Local time: 15:09

Waasi wa Libya wategemea misaada ya kigeni


Wapiganaji waasi nchini Libya wakifyatuliana risasi na majeshi yanayomtii Moammar Gadhafi, nje ya mji wa Kikla, kiasi cha kilomita 40 kutoka mji wa Gheryene nchini Libya

Waasi nchini Libya wanategemea misaada kutoka nchi za nje kusaidia shinikizo lao la kumwondoa madarakani kiongozi wa nchi hiyo Moammar Ghadafi.

Baadhi ya nchi kama vile Ufaransa na Uingereza, zilijitokeza mapema kusaidia upande wa waasi. Uturuki hivi karibuni imeahidi kuwasaidia na nchi nyingine bado hazijaamua. Waziri wa mambo ya nje wa Canada, John Baird, ni mmoja wa wageni waliotembelea karibuni ngome ya waasi nchini Libya katika mji wa Benghazi.

Alisema anatumia ziara hiyo kuonyesha uungaji mkono wa juhudi za waasi za kumwondoa Ghadafi madarakani.

Jalal el Galal, msemaji wa baraza la kitaifa la mpito, ni miongoni mwa wale wanoshukuru msaada wa Canada, ambao Jenerali wake Charles Bouchard, anaongoza operesheni za NATO zinazoungwa mkono na Umoja wa Mataifa za kuwalinda raia wa Libya.Pia anazishukuru nchi ambazo zimelitambua baraza hilo la kitaifa la mpito. Lakini sio nchi zote ambazo ziko tayari kuacha uungaji mkono wa kiongozi wa muda mrefu wa Libya.
Russia na China kwa sababu za kibinafsi zimepinga uingiliaji kati wa nchi za nje katika masuala ya ndani ya nchi zingine.

XS
SM
MD
LG