Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Oktoba 09, 2024 Local time: 12:50

Rais Zelenskyy asema ushindi katika vita utatokana na suluhu ya kidiplomasia

Rais wa Ukraine Volodomyr Zelenskyy alipotembelea eneo la Donetsk mashariki mwa Ukraine,
Rais wa Ukraine Volodomyr Zelenskyy alipotembelea eneo la Donetsk mashariki mwa Ukraine,

Rais wa Ukraine Volodomyr Zelenskyy anasema ushindi katika vita vinavyoendelea nchini mwake na Russia hatimaye utatokana na suluhu ya kidiplomasia.

Rais wa Ukraine Volodomyr Zelenskyy anasema ushindi katika vita vinavyoendelea nchini mwake na Russia hatimaye utatokana na suluhu ya kidiplomasia.

Ushindi utakuwa mgumu, utakuwa na umwagaji damu na katika vita, lakini mwisho wake utakuwa katika diplomasia. Nina hakika sana kuhusu hili,” Zelenskyy alisema katika mahojiano ya televisheni ya Ukraine Ijumaa. "Kuna mambo ambayo hatuwezi kuyamaliza bila kukaa kwenye meza ya mazungumzo."

Kiongozi huyo wa Ukraine pia alisema nchi yake inajaribu kuwaokoa wapiganaji waliojisalimisha kwa vikosi vya Russia baada ya wiki kadhaa za mapigano kwenye kiwanda cha chuma cha Azov-stal katika mji wa bandari wa kusini wa Mariupol.

XS
SM
MD
LG