Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 18, 2024 Local time: 17:37

Rais wa Zimbabwe atakiwa kujiuzulu


Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe akizungumza katika mkutano wa umoja wa mataifa
Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe akizungumza katika mkutano wa umoja wa mataifa

Waziri mkuu Tsvangirai aliwaambia waandishi wa habari Jumatano kwamba inabidi rais Mugabe atafakari juu ya kuacha madaraka kwa ajili na manufaa ya nchi

Waziri mkuu wa Zimbabwe Morgan Tsvangirai ametoa mwito kwa rais Robert Mugabe kuachia madaraka kutokana na hali ya afya yake na umri kubwa.

Kuna taarifa kwamba kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 87 amekuwa akitibiwa ugonjwa wa saratani wa tezi kibofu, lakini hajawahi kuthibitisha hilo hadharani.

Waziri mkuu Tsvangirai aliwaambia waandishi wa habari Jumatano kwamba inabidi rais Mugabe atafakari juu ya kuacha madaraka kwa ajili na manufaa ya nchi, kumbukumbu yake na watoto wake.

Siku ya Jumapili bwana Mugabe alirejea kutoka moja kati ya ziara yake nyingi huko Singapore ambako alifanyiwa matibabu ya ugonjwa ambao haukutajwa.

Aliporejea bwana Mugabe alitangaza kuwa ana hali nzuri ya afya.

Bwana Mugabe aliyetawala Zimbabwe kwa miaka 31 alifikia makubaliano ya kushirikiana madaraka na waziri mkuu Tsvangirai mwaka 2008 baada ya kufanyika uchaguzi ulokuwa mzozo mkubwa. Serikali hiyo imekua ikikabiliwa na matatizo ya utawala tangu kuudwa kwake.

Bwana Mugabe ameahidi kwamba atagombania tena kiti chake katika uchaguzi mwaka ujao.

XS
SM
MD
LG