Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Julai 22, 2024 Local time: 07:17

Rais wa Zambia aonya upinzani

FILE - Zambian police officers apprehend supporters of the opposition United Party for National Development outside the presidential election result center at the Mulungushi International Conference Center in Lusaka, Jan. 21, 2015.

Rais wa Zambia, Edgar Lungu amesema yuko tayari kutumia mbinu zozote kuhakikisha kwamba nchi hiyo ina amani baada ya uchaguzi uliopngwa kufanyika wiki ijayo wa rais, bunge , na serikali za mitaa pamoja na kura ya maoni. Lungu amesema kuwa ana ripoti za kijasusi kuwa wanachama wa chama kikuu cha upinzani , UPND, wanapanga kuzua vurugu iwapo chama chao hakitashinda katika uchaguzi huo.

Lakini kwenye mahojiano na Sauti ya Amerika, naibu wa kiongozi wa chama cha UPND, Canisius Banda, aliikosoa kauli hiyo ya rais Lungu na kuitaja kama ya kupotosha. Alisema rais anaungwa mkono na katiba kuhakikisha kuwa kuna umoja nchini Zambia. Banda hata hivyo alisema kuwa rais huyo anataka kutumbukiza Zambia katika lindi la taharuki na vurugu iwapo atatumia mbinu za kiimla katika juhudi za kutafuta amani.

XS
SM
MD
LG