Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 07, 2022 Local time: 09:02

Rais wa zamani wa Tunisia aaga dunia


Rais wa zamani wa Tunisia Zine El Abidine Ben Ali

Rais wa zamani wa Tunisia Zine el-Abidine Ben Ali amekufa akiwa uhamishoni, familia yake imesema.

Ben Ali aliiongoza nchi hiyo kwa miaka 23 na alikuwa amesifika kwa kuleta utulivu na neema ya kiuchumi.

Lakini alikosolewa na wengi kwa kukandamiza uhuru wa kisiasa na vitendo vya ufisadi vilivyokuwa vimekithiri.

Mwaka 2011, alilazimishwa kuachia madaraka baada ya maandamano makubwa yaliyojiri mitani. Hili lilisababisha wimbi la maandamano kote katika ulimwengu wa Kiarabu yaliyokuwa yakijulikana kama Arab Spring

Nchi zisizopungua nusu darzeni katika eneo hilo la Afrika zilijikuta marais wao wakiondoka madarakani au migogoro kuzuka baada ya kiongozi huyo wa Tunisia kulazimishwa kuachia madaraka, na harakati hizo kupewa jina la Arab Spring.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG