Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 23, 2024 Local time: 23:44

Rais wa zamani wa shirikisho la riadha Kenya, Isaiah Kiplagat, afariki


athletics kenya
athletics kenya

Aliyekuwa rais wa chama cha wanariadha nchini Kenya, Isaiah Kiplagat, aliaga dunia siku ya Jumatano baada ya kuugua saratani kwa muda mrefu.

Kwa mujibu wa gazeti la Daily Nation, Kiplagat alifariki mwendo wa saa nne na nusu akiwa nyumbani kwake mjini Nairobi.

Mwanariadha huyo wa zamani aliongoza shirikisho hilo kwa Zaidi ya miongo mitatu kabla ya kusimamishwa wadhifa wake kufuatia shutuma za rushwa na ukosefu wa uwajibikaji.

Alikuwa na umri wa miaka 72.

XS
SM
MD
LG