Abdel Aziz, mwenye umri wa miaka 66 na jenerali wa zamani wa kijeshi, anakabiliwa na mashtaka ya kupata utajiri kwa njia isio halali katika miaka 11 ya utawala wake.
Alikamatwa mkesha wa kesi yake, amesema wakili wake Cire Cledor Ly.
Polisi “walikuja kumtafuta nyumbani kwake” katika mji mkuu Nouakchott, wakiwa na hati ya kumkamata, walisema.
Vigogo wengine 10 katika utawala wake, wanakabiliwa pia na mashtaka ya ufisadi, utakatishaji wa fedha na utajiri usio halali, walikamatwa pia, chanzo cha usalama kimesema.
Facebook Forum