Rais wa zamani wa Ivory Coast Laurent Gbagbo ameondoka nchini humo Jumatano kuelekea The Hague baada ya mahakama ya kimataifa ya uhalifu kutoa hati ya kumkamata. Wawakilishi wa Gbagbo huko Abidjan walithibitisha Jumanne kuwa kiongozi huyo wa zamani ameondoka nchini humo kwenye ndege maalum kuelekea Uholanzi. Hati hiyo kukamatwa ilipelekwa kwa kiongozi huyo wa zamani mapema Jumanne . Alikuwa kwenye kifungo cha ndani kwenye kijiji kimoja kidogo kaskazini mwa nchi baada ya kutimuliwa madarakani na majeshi ya kimataifa miezi 7 iliyopita. Gbagbo alikatalia madarakani baada ya kushindwa katika uchaguzi uliopita na rais wa sasa Alassane Outtara.
Rais wa zamani wa Ivory Coast aelekea The Hague

Rais Gbagbo apelekwa Uholanzi kwenye mahakama ya ICC baada ya mahakama ya hiyo kutoa hati ya kumkamata.