Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Februari 28, 2024 Local time: 15:40

Rais wa Yemen ajiuzulu


Rais wa zamani wa Yemen, Abd Rabbuh Mansour Hadi akizungumza wakati wa kufunga mashauriano ya kitaifa mjini Sana'a
Rais wa zamani wa Yemen, Abd Rabbuh Mansour Hadi akizungumza wakati wa kufunga mashauriano ya kitaifa mjini Sana'a

Rais wa Yemen Abd Rabbuh Mansour Hadi na baraza lake la mawaziri walielezea kujiuzulu kwao. Hatua hiyo imekuja kufuatia vuguvugu la vita vya kisiasa kati ya Rais na wanamgambo wa Houthi ambao wameshambulia nchi tangu jumatatu.

Msemaji wa serikali ya Yemen mjini Washington, Mohammed Albasha alitangaza Rais wa Yemen aliyekumbwa na matatizo alijiuzulu kupitia mtandao wa kijamii hapo alhamis.

Ikinukuu tolea la Facebook la Waziri Mkuu Khaled Bahah, shirika la habari la Reuters lilimnukuu yeye akisema serikali haitaki kushirikishwa katika njia ya kujenga upya masuala ya kisiasa.

Wapiganaji wa Houthi wakiwa wamezingira makazi ya rais mjini Sana'a
Wapiganaji wa Houthi wakiwa wamezingira makazi ya rais mjini Sana'a

Akizungumza kutoka Sanaa siku ya alhamis mwakilishi wa Umoja wa Mataifa, Jamal Benomar alisema matatizo ya kisiasa yatatatuliwa kama tu makundi ya upinzani yanayoheshimu mikataba ya awali ambayo inatoa wito wa kushirikiana madaraka na kumaliza ghasia.

Chini ya katiba ya Yemen spika wa bunge atahudumu kama rais wa muda nchini humo. Spika wa sasa, Yahia al-Rai ni mshirika wa Rais wa zamani Ali Abdullah Saleh.

Taarifa za barua ya kujiuzulu zilifika kwa majibu ya kimya kimya kutoka kwa msemaji wa wizara ya mambo ya nje Marekani, Jen Psaki.

Bibi Psaki alisema Marekani inaunga mkono uongozi wa muda wa amani nchini Yemen lakini hakuelezea kwa kina juu ya namna uongozi huo wa muda utakavyokuwa.

XS
SM
MD
LG