Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Novemba 10, 2024 Local time: 18:11

Rais wa Yemen apinga mpango wa kujiuzulu


Waandamanaji wanaoipinga serikali wakimtaka Rais Ali Abdullah Saleh, aachie madaraka.
Waandamanaji wanaoipinga serikali wakimtaka Rais Ali Abdullah Saleh, aachie madaraka.

Rais wa Yemen asema pendekezo la kumtaka kujiuzulu ni sawa na mapinduzi ya katiba ya nchi.

Rais wa Yemen ametangaza kuukataa mpango uliopendekezwa na mataifa ya ghuba hivi leo huko maelfu ya waandamanaji wakiwa wamekusanyika katika mji mkuu, Sana'a.

Rais Ali Abdullah Saleh aliwaambia wafuasi kuwa serikali yake imeukataa mpango ambao ameuita ni mapinduzi dhidi ya katiba na demokrasia ya nchi. Amesema mamlaka ya Yemen yametokana na watu wake na siyo kutoka Qatar au kwa mtu mwingine yoyote.

Jana Waziri Mkuu wa Qatar, Sheikh Hamad bin Jassem al-thani amesema baraza la ushirikiano wa ghuba lenye nchi wanachama sita walikuwa na matumaini ya kufikia makubaliano na Bwana Saleh kwa kumtaka ajiuzulu. Makundi ya upinzani yamesema mpango huo unataka kiongozi wa Yemen akabidhi madaraka kwa naibu wake.

Wakitoa sauti zao wale wanaoiunga mkono serikali na waandamanaji wanaoipinga serikali walikusanyika kaitka maeneo tofauti katika mji mkuu hivi leo baada ya sala ya ijumaa.

Kwa muda wa miezi miwili iliyopita, waandamanaji wanaoipinga serikali wamekuwa wakitaka utawala wa Bwana Saleh uliodumu kwa miaka 32 ufikie kikomo. Amekubali kujiuzulu, lakini baada ya uchaguzi mpya kufanyika.

XS
SM
MD
LG