Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 15:15

Rais wa Uturuki ayalaumu mataifa ya magharibi kwa kutoisaidia nchi yake


Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan akizungumza katika mkutano wa usalama, Istanbul, Uturuki, Mei 8, 2016.
Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan akizungumza katika mkutano wa usalama, Istanbul, Uturuki, Mei 8, 2016.

Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan aliyashutumu mataifa ya magharibi ambayo yanapambana na kundi lenye msimamo mkali la Islamic State huko kaskazini mwa Syria kwa kushindwa kuisaidia serikali yake kupambana na wana jihadi kwenye ardhi ya uturuki.

Bwana Erdogan alizungumza Jumapili mjini Instanbul kwamba “wametuacha peke yetu katika mapambano yetu dhidi ya taasisi ya Islamic State, ambayo inamwaga damu zetu kote kupitia mabomu ya kujitoa mhanga na kwa mashambulizi ya roketi ya kukatisha mpaka kwenye mji wa Kilis katika mpaka wa Uturuki”.

Matamshi yake yamekuja siku moja baada ya maafisa kusema makombora ya Uturuki yaliwauwa waasi 55 wa Islamic State kaskazini mwa Syria ikiwa ni majibu kwa wiki kadhaa za mashambulizi ya roketi ambayo yameuwa zaidi ya watu 200 ndani na karibu na mji wa Kilis.

XS
SM
MD
LG