Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Januari 30, 2023 Local time: 02:11

Rais wa Uturuki amefurahishwa na Russia kuwa wazi juu ya vikosi vya Kikurdi kaskazini mwa Syria


Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan (L) na Rais wa Russia Vladimir Putin (R)

Erdogan amekuwa akitishia kuanzisha uvamizi mpya kaskazini mwa Syria ili kuviondoa vikosi vya Kikurdi anavyovilaumu kwa mlipuko wa bomu mwezi Novemba uliosababisha vifo vya watu sita mjini Istanbul

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan alimwambia mwenzake wa Russia Vladimir Putin siku ya Jumapili kwamba ilivutiwa na Kremlin kuwa "wazi" kuhusu vikosi vya Kikurdi kutoka kaskazini mwa Syria.

Erdogan amekuwa akitishia kuanzisha uvamizi mpya kaskazini mwa Syria ili kuviondoa vikosi vya Kikurdi anavyovilaumu kwa mlipuko wa bomu mwezi Novemba uliosababisha vifo vya watu sita mjini Istanbul.

Makubaliano ya mwaka 2019 kati ya Moscow na Ankara yalimaliza mashambulizi mengine kwa kuweka "eneo salama" la kilomita 30 ili kuilinda Uturuki dhidi ya mashambulizi ya mpakani kutoka eneo la Syria.

Erdogan anaishutumu Russia mhusika mkuu katika mzozo wa Syria ambayo inamuunga mkono Rais Bashar al-Assad kwa kushindwa kuheshimu makubaliano hayo.

Erdogan alimwambia Putin kwa njia ya simu kwamba "ni muhimu kuwaondoa wapiganaji wa Kikurdi kutoka mpakani hadi kiwango cha angalau kilomita 30," ofisi yake ilisema.

Erdogan amesema ni "kipaumbele", urais wa Uturuki ulisema.

Baadhi ya vikosi vya Kikurdi viko katika maeneo yaliyo chini ya udhibiti wa jeshi la Russia.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG