Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Agosti 09, 2026 Local time: 22:36

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy atembelea eneo la Kherson

Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelenskyy akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari katika Mkutano wa Jumuiya ya Kisiasa ya Ulaya (EPC) huko Bulboaca, karibu na Chisinau, Moldova, Alhamisi, Juni 1, 2023.
Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelenskyy akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari katika Mkutano wa Jumuiya ya Kisiasa ya Ulaya (EPC) huko Bulboaca, karibu na Chisinau, Moldova, Alhamisi, Juni 1, 2023.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy alisema Alhamisi kwamba alitembelea eneo la Kherson ambako maelfu ya watu wanakabiliana na athari za mafuriko kufuatia uharibifu wa bwawa la Kakhovka.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy alisema leo Alhamisi kwamba alitembelea eneo la Kherson ambako maelfu ya watu wanakabiliana na athari za mafuriko kufuatia uharibifu wa bwawa la Kakhovka.

Zelenskyy alisambaza video kwenye mtandao wa Telegraph akikutana na maafisa na kusema walijadili uhamishaji, kurejesha mfumo wa ikolojia wa mkoa na hali ya kijeshi katika eneo hilo.

Hiyo ilifuatia hotuba yake ya Jumatano usiku ambapo alitoa wito wa jibu la Ulimwengu la wazi na la haraka.

Alisema juhudi kubwa zinahitajika ikiwa ni pamoja na usaidizi wa makundi kama vile Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu.

ICRC ilisema mapema Jumatano ilikuwa ikishirikiana kwa karibu na Shirika la Msalaba Mwekundu la Ukraine ili kuunga mkono mwitikio wa kibinadamu kwa uharibifu wa bwawa hilo.

This item is part of

Forum

XS
SM
MD
LG