Zelenskiy yuko Marekani kutayarisha “mpango wa ushindi” na washirika wake wa karibu, katika juhudi za kuwa na ushawishi katika kupanga sera ya White House kuhusiana na vita vya Ukraine dhidi ya Russia bila kujali nani atashinda uchaguzi wa Novemba.
Kiongozi huyo wa Ukraine amesema anataka kuwasilisha mpango wake kwa rais Joe Biden na wagombea wawili ambao wanaweza kuchukua nafasi yake, Kamala Harris na Donald Trump, wakati wa safari ambayo Zelenskiy atalihutubia baraza kuu la Umoja wa Mataifa siku ya Jumanne.
Zelenskiy amesema kuwa kama mpango utaungwa mkono na nchi za Magraibi, itakuwa na athari kubwa kwa Moscow pamoja na kua na pigo la kisaikologia itakayosaidia pengine kumlazimisha Putin kumaliza vita kwa njia ya kidiplomasia.
Forum