Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 09, 2024 Local time: 20:39

Viongozi katika mkutano wa Umoja wa mataifa wanaangazia usalama na amani


Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres akizungumza mjini New York, September 22, 2024. (Photo by ANGELA WEISS / AFP)
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres akizungumza mjini New York, September 22, 2024. (Photo by ANGELA WEISS / AFP)

Viongozi watafanya kazi pamoja kushughulikia changamoto za kimataifa ikiwemo mabadiliko ya hali ya hewa na migogoro.

Viongozi na wanadiplomasia wanatarajiwa kuhutubia mkutano wa Jumatatu juu ya kuimarisha mfumo wa Umoja wa Mataifa, siku moja baada ya kukubali kufanya kazi pamoja kushughulikia changamoto mbalimbali za kimataifa, ikiwemo mabadiliko ya hali ya hewa, migogoro na umaskini.

Kikao hicho cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kinakuja siku moja kabla ya viongozi wa dunia kuhutubia mkutano wa kila mwaka katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York hapa Marekani.

Mkutano wa Jumatatu unaoangazia uongozi wa baadae umepangwa kujumuisha hotuba kutoka kwa Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy, Rais mpya wa Iran Masoud Pezeshkian, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken, Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi, na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia Sergey Vershinin.

Siku ya Jumapili, wajumbe walitoa idhini ya mwisho kwa Mustakbali wa Baadae, ambao unashughulikia mada kama vile amani na usalama, maendeleo endelevu, ushirikiano wa kidijitali, haki za binadamu na jinsia.

Forum

XS
SM
MD
LG