Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Juni 22, 2024 Local time: 10:13

Rais wa Ukraine atimuliwa na kiongozi wa upinzani apokelewa kama shujaaHali ya utulivu yarudi tena Ukraine baada ya bunge kupiga kura kumondowa madarakani Rais Viktor Yanukovych, mapema Jumamosi.

Baada ya uwamuzi huo wabunge walipiga kura kuamrisha kuachiliwa huru kwa kiongozi wa upinzani na waziri mkuu wa zamani Bi. Yulia Tymoshenko, aliyekuwa katika hospitali ya jela.

Saa chache baadae Bi. Tymoshenko aliwasili kwenye uwanja wa Uhuru mjini Kiev, na kupokelewa kama shujaa alipowahutubia maelfu ya wafuasi wa upinzani, akiwahimiza kuendelea na vita vyao.

Akiwahutubia kutoka kiti cha wagonjwa kutokana na kuumwa sana mgongo,Tymoshenko aliwataja waandamanaji kuwa ni mashujaa na mfano mzuri kwa Ukraine, akiwasifu kwa kuendelea na kampeni yao kabla ya kuanza kutoka machozi.

Akiwa mpinzani mkubwa wa muda mrefu wa Yanukovych, Bi. Tymoshenko alisema kwamba "utawala wa kidikteta umeangushwa," na kutowa heshima zake kwa waandamajani.

Mambo yalibadilika kwa ghafla huko Ukraine kufuatia makubaliano ya kumaliza ghasia na maandamano yaliyofikiwa kati ya serikali na upinzani mwishoni mwa wiki, na hapo tena bunge kupiga kura kumondowa mdarakani rais na kuitisha uchaguzi wa mapema wa rais hapo May 25.
XS
SM
MD
LG