Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amesema kondom za bure zitapatikana katika maduka ya dawa kwa mtu yeyote hadi umri wa miaka 25 kuanzia mwaka ujao.
Hatua hiyo mpya inakuja wakati kasi ya magonjwa ya zinaa na mfumuko wa bei ikiongezeka nchini Ufaransa.
Awali, Macron alitangaza kuwa kondomu hizo zitapatikana kwa watu kati ya umri wa miaka 18 hadi 25, lakini alipata changamoto kwenye mitandao ya kijamii kuhusu kondomu hizo kutopatika kwa vijana wanaobalehe na akaamua kupanua mpango huo kwa mtu yeyote hadi umri wa miaka 25.
Wasichana na wanawake tayari wanapatiwa dawa za bure za uzazi wa mpango nchini Ufaransa.